Video

Siku ya 5 ya uokoaji yagonga mwamba, Likoni

Siku ya 5 ya uokoaji yagonga mwamba, Likoni
Matumaini ya kupata miili ya mama na mtoto wake waliozama baharini yanazidi kudidimia, huku shughuli ya kutafuta gari walilotumbukia nalo majini zaidi ya futi 60 chini ya bahari hindi ikikosa kuzalisha matunda kwa siku ya tano sasa. Kulingana na mpiga mbizi mashuhuri mjini Mombasa Musa Sila, hali halisi kule chini ya bahari ni hatari zaidi kwa waokoaji kuendelea kutafuta gari hilo ambalo kwa sasa, halijulikani lipo katika eneo hilo au la.